1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ndege ya mizigo ya Urusi yadunguliwa huko Sudan

22 Oktoba 2024

Ripoti kutoka ndani ya Urusi zimesema ndege ya kusafirisha mizigo ya Ilyushin Il-76 imedunguliwa katika eneo la magharibi huko Sudan ambako vita kati ya jeshi la serikali na kundi la wanamgambo wa RSF vinaendelea.

Wanapiganaji wa Sudan wa kikosi cha RSF
Wanapiganaji wa Sudan wa kundi la RSFPicha: Rapid Support Forces/AFP

Shirika la habari la serikali la Urusi TASS limeripoti kuwa ubalozi wa nchi hiyo mjini Khartoum unachunguza madai kwamba raia wa Urusi walikuwamo ndani ya ndege hiyo. Kupitia mitandao ya kijamii wawakilishi wa kundi la wanamgambo wa RSF wameripoti kuidungua ndege hiyo. Kituo cha Telegraph cha Urusi, Mash kimeripoti kwamba huenda Warusi wawili walikuwa ndani ya ndege hiyo ya mizigo ingawa hakukuwa na taarifa za kina kuhusu njia, idadi ya watu katika ndege hiyo. Sudan ambayo ni nchi ya tatu kwa ukubwa barani Afrika imetumbukia kwenye vita vya wenyewe kwa zaidi ya mwaka sasaambapo mamilioni ya watu wake wamekyakimbia makazi yao kufuatia vita hivyo.