Ndege ya shirika la ndege la Uturuki yatekwa nyara
18 Agosti 2007Matangazo
Ankara:
Ndege ya Abiria ya Uturuki imetekwa nyara ilipokua njiani toka kaskazini mwa kisiwa cha Cyprus kuelekea Istanbul nchini Uturuki.Ndege hiyo ya shirika la ndege la “Atlas Jet” imetuwa katika uwanja wa ndege wa Antalya.Wengi kati ya abiria 136 wamefanikiwa kujisalimisha.Wateka nyara wote wawili wanaozungumza kiarabu wanadai kua wafuasi wa mtandao wa kigaidi wa al Qaida.Kwa mujibu wa vyombo vya habari wateka nyara hao wanataka ndege hiyo ya Uturuki ielekee Iran au Syria.