Ndege yaanguka majini Parlem.
6 Agosti 2005Matangazo
Habari tulizozipata hivi punde zinasema kuwa ndege moja ya abiria ya shirika la ndege la Tunisia ambayo inauwezo wa kubeba abiria 50 imeanguka katika bahari karibu na mji wa Parlemo katika kisiwa cha Sicily nchini Italia leo, shirika la habari la ANSA limeripoti likiwakariri wafanyakazi wa jeshi la zima moto.
