Ndege za Israel zashambulia kusini mwa Lebanon
20 Machi 2026
Matangazo
Israeli ilifanya mashambulizi katika miji iliyo kusini mwa Lebanon, na kusababisha watu wengi kujeruhiwa. Hayo yameripotiwa na vyombo vya habari vya serikali Ijumaa.
Shirika rasmi la habari la kitaifa la Lebanon limeripoti kamba ndege za kivita za adui Israeli zilishambulia alfajiri, zikiilenga miji ya Bafliyeh na Hanine katika wilaya za Tyre na Bint Jbeil na kuongeza kuwa vikosi vya Israel vilikuwa vimeishambulia miji mingine mitano kusini mwa nchi.