N’DJAMENA : Wanaosafirisha watoto kimagendo kuadhibiwa
27 Oktoba 2007Matangazo
Rais Idris Derby wa Chad ameapa hapo jana kwamba raia tisa wa Ufaransa waliokamatwa kwa kujaribu kuwasafirisha kwa magendo watoto wa Kiafrika kwenda kuishi na familia za kizungu wataadhibiwa kwa uhalifu wao huo muovu kabisa.
Polisi ya Chad ililikamata kundi hilo wakati likijiandaa kuwasafirisha kwa ndege watoto 103 wenye umri kati ya miaka 3 hadi minane wengi wao kutoka jimbo lenye mzozo la Dafur nchini Sudan kupitia mji wa mashariki wa Chad wa Abeche kwa kutumia ndege ya kukodiwa ya Ufaransa.
Wizara ya mambo ya nje ya Uhispania imesema hapo jana Wahispania saba wanaume watatu na wanawake wanne pia wamekamatwa kwa kuhusika kwao na ukodishaji wa ndege hiyo.