1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiEthiopia

Ndoa za utotoni na unyanyasaji vyaongezeka Ethiopia

9 Februari 2023

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Watoto, UNICEF, limefahamisha kuwa ndoa za utotoni, na unyanyasaji wa kijinsia umeongezeka nchini Ethiopia.

Indien Koderma | Kinderarbeit
Picha: DIBYANGSHU SARKAR/AFP/Getty Images

Madaktari na wafanyakazi wa umma wamebaini kuwa kukithiri kwa hali hiyo kutokana na ukame unaosababisha njaa na kuzidi kwa umasikini miongoni mwa raia.

Kwa familia nyingi zilizokata tamaa, kumuoza binti yao ni sawa na kupunguza gharama na mahari inayotolewa husaidia katika matumizi mbalimbali.

UNICEF inasema ndoa za utotoni, ambazo ni kinyume cha sheria nchini Ethiopia, zimeongezeka maradufu katika maeneo manne yaliyoathirika zaidi na ukame katika kipindi cha miezi sita ya kwanza ya mwaka 2022 ikilinganishwa na mwaka uliopita.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW