1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNepal

Nepal yakata tamaa ya kupata manusura wa ajali

16 Januari 2023

Nchini Nepal matumaini ya kupata manusura baada ya ajali ya ndege iliyokuwa imebeba abiria 72 yameondoka.

Nepal | Flugzeugabsturz in Pokhara
Picha: Stringer/REUTERS

Hayo yameelezwa na mmoja wa maafisa waandamizi nchini humo aliyezungumza na shirika la habari la AFP baada ya miili 68 kupatikana hadi sasa kufuatia ajali hiyo iliyotokea jana Jumapili. Afisa mkuu katika eneo la Taksi ilikotokea ajali hiyo Tek Bahandur KC amesema wanaendelea kuitafuta miili ya watu wengine wanne na wanaomba itokee miujiuza ingawa matumaini ya kumpata yeyote akiwa hai yameondoka. Msemaji wa mamlaka ya safari za anga ya Nepal amesema kifaa cha kurekodi data na sauti kimeshapatikana kwenye eneo la ajali. Maombolezo ya siku moja yamefanyika leo nchini humo. Ndege ya shirika la ndege la Yeti ya nambari za usajili ATR 72 iliangukia kwenye korongo na kupasuka vipande na kuripuka moto.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW