SiasaIsrael
Netanyahu aenda Marekani kuujadili mpango wa nyuklia wa Iran
10 Februari 2026
Matangazo
Israel inashinikiza makubaliano hayo yajumuishe Iran kusitisha urutubishwaji wa aina yoyote wa madini ya urani, kupunguza mipango yake ya makombora na kuacha kuwasaidia makundi ya wanamgambo kama ya Hamas na Hezbollah.
Lakini Iran inayapinga masharti hayo na kusema itakubaliana tu na kiwango fulani cha ukomo kwenye mpango wa nyuklia ili badala yake iondolewe vikwazo vya kiuchumi.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Iran Esmail Baqaei mapema leo ameilaumu Israel kwa kupinga kila mchakato wa kidiplomasia unaolenga kuleta amani ya kikanda.