1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Netanyahu afanyiwa upasuaji kabla ya mjadala wa bunge

Sylvia Mwehozi
23 Julai 2023

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amefanyiwa upasuaji wa moyo wa kupandikizwa kifaa cha Pacemaker, kuelekea mjadala wa bunge wa mageuzi tata ya mahakama ambayo yamechochea maandamano makubwa.

Israel- Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin NetanyahuPicha: Abdulhamid Hosbas/AA/picture alliance

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amefanyiwa upasuaji wa moyo wa kupandikizwa kifaa cha Pacemaker, kuelekea mjadala wa bunge wa mageuzi tata ya mahakama ambayo yamechochea maandamano makubwa.Taarifa zaidi kutoka Hospitali zinasema afya yake imeimarika baada ya upasuaji huo uliofanyika usiku wa kuamkia leo.

Mageuzi ya mahakama yanayopendekezwa na serikali ya Netanyahu yenye misimamo mikali ya mrengo wa kulia yameligawa taifa hilo na kuibua mojawapo ya vuguvugu kubwa la maandamano katika historia ya Israel tangu mwezi Januari. Wabunge nchini humo wanatarajiwa hii leo kuujadili bungeni muswada wa marekebisho ya mahakama na kisha kuupigia kura kesho Jumatatu.Netanyahu asitisha mpango tata wa mageuzi ya mahakama

Serikali ya Netanyahu inapanga kudhibiti mamlaka ya Mahakama ya Juu ikisema kwamba mageuzi hayo ni muhimu ili kuhakikisha uwiano bora wa mamlaka. Wapinzani wanasema mageuzi hayo ni kitisho kwa demokrasia ya Israel.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW