1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Netanyahu ailaumu Hamas kwa kuvunja makubaliano

24 Desemba 2025

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameshutumu Hamas kwa kukiuka makubaliano ya kusitisha mapigano Gaza baada ya afisa wa jeshi kujeruhiwa na kifaa cha mlipuko huko Rafah, na Israel ikaapa kulipiza kisasi.

Jerusalem | Benjamin Netanyahu
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aishutumu Hamas kwa kukiuka makubaliano. Picha: Menahem Kahana/AFP

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Netanyahu imesema, Hamas lazima itekeleze kikamilifu makubaliano ya Oktoba, ikibainisha kuwa makubaliano hayo yanatarajia kundi hilo la wanamgambo kuondolewa madarakani Gaza pamoja na kulipokonya silaha na kuondoa misimamo mikali katika eneo hilo. 

Vurugu zimepungua lakini hazijaisha tangu kusitishwa kwa mapigano kuanza tarehe 10 Oktoba, na pande zote zimekuwa zikishutumiana mara kwa mara kwa kukiuka makubaliano hayo. Wizara ya afya ya Gaza inasema Israel imewaua zaidi ya watu 400 katika eneo hilo tangu usitishaji mapigano uanze.

Mpango wa vipengele 20 uliotolewa na Rais wa Marekani Donald Trump mwezi Septemba unatoa wito wa usitishaji wa awali wa mapigano ukifuatiwa na hatua kuelekea amani pana.

Pande hizo hazijakubaliana kikamilifu juu ya vipengele vyote. Hamas imesema itakubali kuachana na silaha ikiwa taifa la Palestina litakuwa huru.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW