Netanyahu aionya Hizbullah dhidi ya kujiingiza vitani
22 Oktoba 2023Matangazo
Netanyahu aliyasema hayo alipowatembelea wanajeshi wake kaskazini mwa Israel karibu na mpaka wa Lebanon siku ya Jumapili (Oktoba 22).
Waziri mkuu huyo aliongeza kuwa kundi hilo la wanamgambo lililo na mafungamo na kundi la Hamas "litafanya makosa makubwa katika maisha yake litakapofikiria kuanzisha vita na Israel."
Soma zaidi: Scholz asikitishwa na kuenea visa vya chuki kwa Wayahudi
Wakati hayo yakiarifiwa, Shirika la Umoja wa Mataifa linalosaidia wakimbizi wa Palestina (UNRWA) limesema malori aita ya chakula yaliingia mjini Gaza tangu vita vilipoanza Oktoba 7.
Malori hayo pia yalikuwa yamebeba mafuta ambayo yangelitumiwa kuwashia mitambo ya majenerata katika hospitali mbili katika eneo hilo.