1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiIsrael

Netanyahu aionya mahakama ya juu

28 Julai 2023

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ametahadharisha kuwa nchi hiyo inaweza kutumbukia kwenye "eneo lisilojulikana" iwapo Mahakama ya Juu itabatilisha sheria mpya ya mahakama.

Israel | Justizreform Abstimmung | Israels Ministerpräsident Benjamin Netanyahu
Picha: Amir Cohen/REUTERS

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ametahadharisha kuwa nchi hiyo inaweza kutumbukia kwenye "eneo lisilojulikana" iwapo Mahakama ya Juu itabatilisha sheria mpya inayoiondolea mahakama hiyo uwezo wa kuzuia utekelezaji wa maamuzi ya serikali.

Katika mahojiano na televisheni ya CNN ya Marekani, Netanyahu amesema anatumai Israel haitofuata mkondo huo bila ya kueleza iwapo serikali yake itauheshimu uamuzi wa mahakama ya juu.

Serikali ya mseto wa vyama vya itikadi kali za kidini na mrengo mkali wa kulia inaituhumu mahakama kwa kuwa na ushawishi mkubwa juu ya maamuzi ya kisiasa, hivyo basi wanataka kupunguza nguvu zake.

Sheria hiyo mpya inawazuia majaji kuainisha maamuzi yanayotolewa na serikali au mawaziri kama "yasiyofaa."

Israel haina katiba rasmi iliyoandikwa na badala yake inategemea mkusanyiko wa sheria za msingi kuiendesha nchi.