1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Netanyahu aitaka Qatar iwafukuze viongozi wa Hamas

11 Septemba 2025

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, ameitaka Qatar kuwaondoa wawakilishi wa wanamgambo wa Hamas nchini humo, siku moja baada ya kuwalenga wakuu wa kundi hilo mjini Doha.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin NetanyahuPicha: Amos Ben Gershom/Israel Gpo/ZUMA/picture alliance

Netanyahu ameituhumu Qatar kwa kulifadhili kundi hilo na kuwapa wakuu wake makao salama na ya kifahari.

"Marekani ilifanya nini baada ya tukio la Septemba 11? Iliahidi kuwasaka magaidi waliofanya uhalifu uhalifu huo, popote walipo. Ilipitisha pia azimio katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, wiki mbili baadae, lililosema serikali hazitowapa makao magaidi. Na sasa naiambia Qatar na mataifa yote yanayowapa makao magaidi, ama muwafurushe au muwafungulie mashtaka, kwa sababu musipofanya hivyo, sisi tutafanya," alisema Netanyahu.

Wizara ya mambo ya kigeni ya Qatar imeyakosoa matamshi ya Netanyahu ikisema ni kitisho cha wazi cha kuingilia uhuru wa baadae wa taifa huru na kudai kuwa ni jaribio la aibu la kuhalalisha shambulizi la Israel mjini Doha hapo Jumanne.

Shambulizi hilo la Israel limelaaniwa na mataifa ya Kiarabu, China na viongozi wa Ulaya.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW