Netanyahu yupo Marekani kujadili usitishaji vita Gaza
7 Julai 2025
Hii ni ziara ya Tatu ya Netanyahu nchini humo tangu Rais wa nchi hiyo Donald Trump alipoingia madarakani miezi sita iliyopita.
Donald Trump amewaambia waandishi habari mjini New Jersey kwamba, anaamini mpango wa kusitisha mapigano na hatua ya kuwaachia mateka wanaoshikiliwa na wanamgambo wa Hamas huenda ukafikiwa wiki hii.
Wapalestina zaidi ya 30 wauawa Ukanda wa Gaza
Ziara ya Netanyahu nchini Marekani inafanyika chini ya wiki mbili baada ya kumalizika vita vilivyodumu kwa siku 12 kati ya Israel na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambako mashambulizi ya Israel na Marekani yaliharibu kinu muhimu cha nyuklia cha Iran.
Netanyahu amesema mashambulizi hayo yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 900 kulingana na maafisa wa Iran yatawezesha kutanua juhudi za amani kuliko ilivyokuwa zamani.