1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Netanyahu amuadhibu waziri wake kwa matamshi dhidi ya Gaza

5 Novemba 2023

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amemuadhibu mwanachama wa ngazi ya chini katika Baraza lake la Mawaziri, aliyesema taifa hilo liko tayari kuchukua hatua ya kurusha bomu la nyuklia katika Ukanda wa Gaza.

Waziri MKuu wa Israel Benjamin Netanyahu amuadhibu waziri wake kwa matamshi dhidi ya Gaza
Waziri MKuu wa Israel Benjamin Netanyahu amuadhibu waziri wake kwa matamshi dhidi ya GazaPicha: imago images/Xinhua

Kupitia taarifa ya ofisi ya Netanyahu, Waziri huyo wa turathi Amihay Eliyahu kutoka chama cha siasa kali za mrengo wa kulia, katika serikali ya muungano amesimamishwa kwa muda katika mikutano ya baraza hilo.

Eliyahu alipoulizwa katika mahojiano na radio moja nchini humo kuhusu uwezekano wa kutupa bomu la nyuklia Gaza, alisema hiyo ni njia moja ya kuwaondoa kabisa watu wa Gaza aliyowaita washirika wa Hamas.

Ofisi ya Netanyahu imesema matamshi ya Waziri huyo hayana nafasi kwa hali halisi inayoendelea sasa na kwamba Israel inatekeleza mashambulizi yake kwa kuzingatia sheria ya kimataifa.

Msemaji wa kundi la Hamas amesema matamshi ya Eliyahu yanawakilisha kile alichosema ni ugaidi wa Israel unaotoa kitisho kwa kanda nzima na dunia kwa ujumla.