1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Netanyahu aomba msamaha kwa rais, ufisadi dhidi yake

1 Desemba 2025

Ombi la Netanyahu kupata msamaha wa rais kuhusu kesi za ufisadi dhidi yake laibua hisia mseto Israel.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin NetanyahuPicha: Abir Sultan/Pool/AFP/Getty Images

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ametuma maombi rasmi ya kutaka msamaha wa rais wa nchi Isaac Herzog, kuhusiana na kesi inayoendelea dhidi yake ya ufisadi, ambayo imeigawa nchi hiyo kwa muda mrefu.

Ombi hilo liliibua upinzani mkali Jumapili kutoka kwa wanasiasa wa upinzani na mashirika yanayokosoa serikali, lakini baadhi ya Waisraeli waliashiria kuliunga mkono.

Ofisi ya Rais Herzog ililitaja ombi hilo kuwa la ‘kipekee' na lenye ‘athari kubwa', hasa kuhusu sifa ya mfumo wa sheria nchini Israel na pia uwepo wa Netanyahu mamlakani.

Netanyahu ndiye Waziri Mkuu pekee wa Israel kuwahi kushtakiwa katika historia ya nchi hiyo.

Anakabiliwa na mashtaka ya ufisadi, kuvunja uaminifu na kukubali rushwa katika kesi tatu tofauti.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW