1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIran

Netanyahu aonyesha mshikamano na wananchi wa Iran

5 Januari 2026

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameonyesha mshikamano na wananchi wa Iran na kueleza uwezekano wa kutokea kwa mabadiliko makubwa nchini humo.

Israel | Jerusalem 2022 | Benjamin Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin NetanyahuPicha: Menahem Kahana/AFP

Akizungumza mwanzoni mwa kikao cha kila wiki cha Baraza la Mawaziri mjini Jerusalem, Netanyahu amesema Israel inasimama pamoja na mapambano ya wananchi wa Iran na matarajio yao ya uhuru, haki na demokrasia.

Kauli ya Waziri Mkuu huyo ameitoa wakati maandamano makubwa yanaendelea kushuhudiwa nchini Iran, ambapo raia wamekuwa wakilalamikia hali ngumu ya kiuchumi.

Katika maelezo yake, Netanyahu pia amesema huenda dunia ikashuhudia wakati ambao wananchi wa Iran wanachukua kile alichokiita hatma yao mikononi mwao.

Mwaka uliopita, Israel iliingia kwenye mzozo na Iran uliodumu kwa muda wa siku 12, na kwa ushirikiano na Marekani ilifanya mashambulizi yaliyolenga baadhi ya vituo muhimu vya nyuklia vya Jamhuri hiyo ya Kiislamu.

Israel imeendelea kuushutumu uongozi wa Tehran kwa kile inachodai ni mpango wa kutengeneza silaha za nyuklia, jambo inaloliona kuwa tishio kwa usalama wake.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW