1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Netanyahu apongeza kuokolewa kwa rubani wa Marekani

5 Aprili 2026

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amempongeza leo Rais wa Marekani Donald Trump kwa kufanikisha operesheni ya kumuokoa rubani mmoja wa ndege ya kivita ya Marekani iliyodunguliwa na Iran.

Israel Jerusalem 2026 | Benjamin Netanyahu katika mkutano na waandishi wa habari mnamo Machi 19, 2026 mjini Jerusalem.
Waziri mkuu wa Israel, Benjamin NetanyahuPicha: Ronen Zvulun/REUTERS

Katika hotuba iliyorekodiwa, Netanyahu amesema Waisraeli wote wanafurahia uokoaji huo wa ajabu wa rubani wa Marekani aliyemuita shujaa.

Ameongeza kusema operesheni hiyo ya uokoaji inatilia mkazo kanuni takatifu kwamba hakuna anayeachwa nyuma.

Katika hatua nyingine makundi ya kujihami yanayoiunga mkono Iran yamefanya mashambulizi mawili usiku wa kuamkia leo dhidi ya maeneo ya kidiplomasia ya Marekani nchini Iraq. Haya yamesemwa leo Jumapili na ubalozi wa Marekani nchini Baghdad.

Kwengineko mamlaka katika Umoja wa Falme za Kiarabu imeripoti uharibifu uliofanyika katika kiwanda cha petrokemikali cha Borouge, baada ya kuanguka kwa vifusi kutoka mifumo ya ulinzi wa anga.

Hakuna majeruhi walioripotiwa .

Mapema, mamlaka ilisema kuwa operesheni katika kiwanda hicho zilikatizwa kwasababu ya kuzuka kwa moto huo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW