1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Netanyahu: Israel inajiandaa kwa mashambulizi zaidi Gaza

11 Aprili 2024

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema Israel inaendeleza vita vyake Gaza lakini pia inajiandaa kwa matukio mengine, wakati kukiwa na wasiwasi kuwa Iran inajiandaa kuishambulia Israel

Benjamin Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu Picha: Maxim Shemetov/REUTERS

Akizungumza baada ya ziara yake katika kituo cha jeshi la angani cha Tel Nof kusini mwa Israel, Netanyahu amesema wako tayari kwa yeyote atakayeidhuru Israel.

"Tunaendelea na juhudi zetu ambazo hazitasimama ili kuwarejesha mateka wetu, lakini pia tunajiandaa na changamoto kutoka kwa maeneo mengine. Tunaweka kanuni iliyo wazi kwamba yeyote anayetudhuru, nasi tutamdhuru. Tunajiandaa kuyakidhi mahitaji yetu ya usalama wa taifa la Israel katika kujilinda na pia katika kushambulia." 

Haniyeh: Vifo vya wananagu Israel inajidanganya

Israel haikusema kama ilihusika na mauaji ya jenerali mmoja wa Iran na maafisa wengine sita katika shambulizi la angani lililoupiga ubalozi mdogo wa Iran katika mji mkuu wa Syria, Damascus mnamo Aprili mosi.

Kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khemenei alisema Israel lazima iadhibiwe kwa kufanya shambulizi hilo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW