1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Netanyahu atarajiwa kutangaza serikali mpya ya Israel

21 Desemba 2022

Mwanasiasa mkongwe wa Israel Benjamin Netanyahu anatarajiwa hivi leo kutangaza kuwa amefanikiwa kuunda serikali mpya na washirika wake wa siasa kali za mrengo wa kulia.

Symbolbild I  Israel: Prime Minister Benjamin Netanyahu am Telefon
Picha: Koby Gideon/ZUMA/IMAGO

Mwanasiasa mkongwe wa Israel Benjamin Netanyahu anatarajiwa hivi leo kutangaza kuwa amefanikiwa kuunda serikali mpya na washirika wake wa siasa kali za mrengo wa kulia, lakini huenda akaomba kurefushwa kwa muda wa mazungumzo yake magumu ya muungano na kambi hiyo.

Kufuatia ushindi wake katika uchaguzi wa Novemba 1, Netanyahu alipewa mamlaka ya kuunda serikali ambayo inatarajiwa kuwa ya mwelekeo wa siasa kali  zaidi za mrengo wa kulia ambayo haijawahi kushuhudiwa katika historia ya Israel.

Muda aliyoongezewa Netanyahu na Rais wa Israel Isaac Herzog ili kuunda serikali mpya utafikia kikomo leo usiku.

Serikali ya Netanyahu mwenye umri wa miaka 73 na aliyeongoza kwa muda mrefu zaidi nchini humo, itachukua nafasi ya muungano wenye itikadi tofauti unaoongozwa na Waziri Mkuu wa sasa Yair Lapid.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW