1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Netanyahu atoa wito wa umoja katikati mwa maandamano ya umma

27 Machi 2023

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ametoa wito hii leo wa kudumisha umoja na kukemea vurugu, wakati maandamano makubwa yakiendelea nchini humo ili kupinga mpango wake wa mageuzi ya mfumo wa mahakama.

Israel Protest gegen die Justizreform/Netanjahu im Parlament
Picha: Ronen Zvulun/REUTERS

Mzozo wa kisiasa wa Israel umeongezeka kufuatia kufutwa kazi Waziri wa Ulinzi Yoav Gallant baada ya kumkosoa Netanyahu juu ya mpango huo wa mageuzi yenye utata na yanayopingwa vikali nchini humo.

Mpango huo ambao ungeliwapa uwezo mkubwa wanasiasa na kupunguza jukumu la Mahakama ya Juu, umetiliwa shaka na washirika wakuu wa Israel ikiwa ni pamoja na Marekani, huku wapinzani wakisema kuwa mpango huo unahatarisha demokrasia ya Israel.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW