Netanyahu awashtumu waliolitambua taifa la Palestina
26 Septemba 2025
Matangazo
Akilihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, kiongozi huyo wa Israel alishtumu hatua za kidiplomasia za washirika wakuu wa Marekani zinazozidisha kutengwa kimataifa kwaIsraeli kwa hatua zake katika vita na kundi la wanamgambo la Hamas.
Netanyahu ameongeza kuwa, viongozi wa Ufaransa, Uingereza, Australia, Canada na mataifa mengine yalilitambua taifa la Palestina baada ya mambo ya kutisha yaliofanywa na Hamas mnamo Oktoba 7, mambo anayodai yalipongezwa na asilimia 90 ya Wapalestina.
Kiongozi huyo pia amesema viongozi wengi wanaomshtumu hadharani wanampongeza faraghani.