1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Netanyahu: Israel inaelekea kukamilisha operesheni yake Gaza

24 Juni 2024

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kuwa awamu ya sasa ya mapigano dhidi ya Hamas huko Gaza inaelekea kumalizika.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.Picha: Ohad Zwigenberg/AP/dpa/picture alliance

Hii inatoa nafasi kwa Israel kuwapeleka askari zaidi kwenye mpaka wake wa kaskazini ili kukabiliana na kundi la wanamgambo wa Lebanon, la Hezbollah.

Kiongozi huyo wa Israel alisema katika mahojiano marefu ya televisheni ya nchini humo kuwa ingawa jeshi linakaribia kukamilisha operesheni yake ya ardhini katika mji wa Rafah, kusini mwa Gaza, lakini haimaanishi  kuwa vita dhidi ya Hamas vimemalizika. 

Matamshi ya Netanyahu yanatishia kuongeza mvutano zaidi kati ya Israel na Hezbollah katika wakati ambao pande hizo mbili zinaonekana kukaribia kuanzisha vita.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW