1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Netanyahu kukutana na baraza lake la usalama kujadili Hamas

4 Julai 2024

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anatarajiwa kufanya mkutano na baraza lake la usalama kujadili misimamo mipya ya kundi la wanamgambo la Hamas kuhusu makubaliano ya kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
Netanyahu atashauriana na kundi la wawakilishi wake kwenye mazungumzo ya kusitisha mapigano.Picha: Cohen-Magen/REUTERS

Chanzo katika ofisi ya Netanyahu kimearifu kuwa kabla ya kukutana na baraza hilo, Waziri Mkuu huyo atashauriana na kundi la wawakilishi wake kwenye mazungumzo ya kusitisha mapigano.

Israel ilipokea majibu ya Hamas jana Jumatano kwa pendekezo lililotangazwa hadharani mwishoni mwa mwezi Mei na Rais wa Marekani Joe Biden ambalo linajumuisha kuachiliwa kwa mateka wapatao 120 wanaoshikiliwa hukoGaza na kusitishwa kwa mapigano katika ukanda huo.

Afisa mmoja wa Palestina aliye karibu na juhudi za upatanishi ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba kundi la Hamas limeonesha kuwa tayari kurekebisha baadhi ya matakwa yake hatua itakayofungua njia ya kupatikana mkataba wa kusitisha mapigano iwapo Israel itaridhia.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW