1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Netanyahu na Biden wajadili kuhusu mazungumzo ya Doha

13 Januari 2025

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amezungumza na Rais wa Marekani Joe Biden kuhusu "maendeleo" yaliyopigwa kuhusu makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na kundi la wanamgambo la Hamas.

Marekani | Washington 2024 | Biden
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Rais wa Marekani Joe BidenPicha: Susan Walsh/AP Photo/picture alliance

Makubaliano hayo pia yanalenga kuachiliwa huru kwa mateka wanaoshikiliwa na Hamas katika ukanda wa Gaza na Wapalestina walioko katika magereza ya Israel.

Netanyahu amemwambia Biden kuhusu jukumu aliloipa timu inayoshiriki mazungumzo hayo mjini Doha ili kuendeleza juhudi za kuachiliwa huru mateka, na pia amewashkuru Biden na Rais mteule Donald Trump kwa msaada wao katika kufanikisha hilo.

Soma pia: Israel yaua dazeni kadhaa Gaza katikati mwa juhudi za kumaliza vita

Ikulu ya Marekani imeeleza kwamba, Biden na Netanyahu walijadili juu ya mazungumzo yanayoendelea mjini Doha na kuachiliwa kwa mateka kwa kuzingatia mpango wa kusitisha mapigano uliowasilishwa na Biden mnamo mwezi Mei mwaka uliopita.

Kulingana na taarifa ya Ikulu ya Marekani, viongozi hao wawili walizungumza pia kuhusu mazingira ya kikanda yaliyobadilika kufuatia hatua ya kusitishwa mapigano nchini Lebanon, kuanguka kwa utawala wa Assad nchini Syria na kudhoofika kwa ushawishi wa Iran katika eneo hilo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW