1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Je, Hamas ndiyo itakuwa mwisho wa kisiasa wa Netanyahu?

30 Novemba 2023

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesimama njia panda akikabiliwa na vita dhidi ya kundi Hamas na upinzani ndani ya kisiasa nchini mwake. Amekosolewa vikali kushindwa kuzuwia mashambulizi ya Hamas, Oktoba 7.

Israel Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alipotembelea Ukanda wa Gaza, wakati wa mapatano ya muda ya kusitisha vita, Novemba, 26, 2023.Picha: Avi Ohayon/GPO/Handout via REUTERS

Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu alifuatilia kuachiliwa kwa mara ya kwanza kwa mateka wanaoshikiliwa na Hamas, huku familia zao zikisubiri mjini Tel Aviv karibu na Benny Gantz, mpinzani wake wa karibu.

Gantz, mkuu wa zamani wa jeshi na kiongozi wa upinzani ambaye alijiunga na baraza la mawaziri la vita la Netanyahu mwezi uliopita, aliwaomba waandishi wa habari wa Televisheni kumuacha pekeyake na familia hiyo.

Picha zilizochapishwa baadaye zilimuonyesha akiwakumbatia watu katika umati na kwa upande mwengine Netanyahu alitazama akiwa katika makao makuu ya ulinzi.

Huku akikabiliwa na wimbi kubwa la ukosoaji juu ya kushindwa kwake kuzuia mzozo dhidi ya Hamas kujipenyeza Israel mnamo Oktoba 7, Netanyahu kwa kiasi kikubwa amekwepa kuonekana hadharani wakati akiendesha vita vya pande mbili, mmoja dhidi ya Hamas na mwingine kwa ajili ya uhai wake kisiasa.

Waziri Mkuu Netanyahu akiwa na wanajeshi wake katika Ukanda wa Gaza wakati wa usitishaji wa muda mfupi wa mapigano, Novemba, 26,2023.Picha: Avi Ohayon/GPO/Handout via REUTERS

Netanyahu, mwenye umri wa miaka 74, kwa muda mrefu ameonesha kuwa mlinzi wa usalama, akiwa thabiti dhidi ya Iran na kuungwa mkono na jeshi lililohakikisha kwamba kamwe Wayahudi hawataingia tena kwenye mashaka lakini ame kakabiliwa na tukio baya zaidi katika Israeli tukio baya zaidi katika hiyoria ya miaka 75 ya Israel.

Kushindwa kulinda mipaka ya taifa

Waisraeli wamewaepuka baadhi ya mawaziri wa baraza la mawaziri la Netanyahu wakiwalaumu kwa kushindwa kuwazuia wapiganaji wa Hamas kutoka Gaza kufanya shambulizi la kushtukiza na kusababisha vifo vya watu 1,200, kuwateka nyara wengine 240 na kuiingiza nchi katika vita.

Soma pia: Fahamu zaidi kuhusu mateka wa Israel chini ya Hamas

Katika matukio tofauti, takriban mawaziri wake watatu katika baraza la mawaziri la Israel walidhihakiwa na kunyanyaswa walipojitokeza hadharani, hatua iliyodhihirisha ukubwa wa hasira ya umma.

Netanyahu yumkini anafaidika katika vita vinavyoendelea kwani vinachelewesha zaidi kesi yake ya ufisadi ya miaka 3 na nusu na kuahirisha uchunguzi wa serikali unaotarajiwa kufuatilia kwa nini Israeli chini ya uongozi wake ilikabiliwa na shambulizi la kushtukiza.

Akikabiliana na majenerali, anaweza pia kuwa na matumaini ya kuokoa sifa zake kupitia mwenendo wake wa vita na kurudi kwa mateka huku akikataa kuwajibika na kukataa pia kujibu swali katika mkutano wa nadra wa wanahabari alioulizwa ikiwa atajiuzulu.

Mashambulizi ya Hamas yalitokea wakati Netanyahu akikabiliana na upinzani mkali nyumbani kuhusiana na mageuzi ya sheria ya mahakama.Picha: Jack Guez/AFP/Getty Images

Netanyahu ameapa kudhibiti usalama huko Gaza kwa muda usiojulikana, na kuongeza kutokuwa na uhakika kwa hatima ya taifa hilo ambapo kwa muda wa wiki saba Israeli imekuwa kwenye mashambulizi kabla ya kufikia makubaliano ya muda na Hamas ya kuwaachilia mateka na kubadilishana wafungwa.

Je, atanusurika safari hii au ndiyo mwisho?

Waziri mkuu huyo aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi wa Israel, amewahi kunusurika katika mizozo mingi ya kisiasa, akifanya mabadiliko kadhaa, na hahitaji kukabiliwa na uchaguzi mwingine kwa miaka mitatu ikiwa muungano wake utabakia kuwa dhabiti.

Soma pia:Netanyahu apuuza miito ya washirika kuwalinda raia wa Gaza 

Kwa upande mwengine mpizani wake mkuu Gantz, mwenye umri wa miaka 64, aliyejiunga na baraza la mawaziri la vita la Israel ambalo Netanyahu aliunda baada ya shambulio la Hamas ili kuiunganisha nchi katika kampeni ya kukabilina na Hamas na kurejesha mateka.

Akiwa na uzoefu wa karibu miaka 40 katika jeshi, Gantz kutoka chama cha mrengo wa kati anampa Netanyahu na chama chake cha mrengo wa kulia cha Likud msimamo thabiti zaidi kwa serikali ambayo inapunguza ushawishi wa mrengo wa kulia na washirika wa muungano wa kidini kwenye ukingo wa jamii ya Israeli. Mahasimu hao wanaungana katika vita lakini wanatofautia katika misimamo ya kisiasa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW