1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Netanyahu na Zelensky ziarani Marekani

28 Julai 2026

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky wanatarajiwa kuwasili Jumanne mjini Washington kuhudhuria ibada ya mazishi ya seneta wa chama cha Republican Lindsey Graham.

Rais Trump, Zelensky na Waziri Mkuu wa Israel B.Netanyahu
Kutoka kushoto: Rais Donald Trump wa Marekani, Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin NetanyahuPicha: picture alliance

Viongozi hao watatumia pia fursa hiyo kukutana na Rais wa Marekani Donald Trump. Graham aliyefariki Julai 11 akiwa na umri wa miaka 71, alikuwa mmoja wa washirika na watetezi wakubwa wa Israel na Ukraine huko Washington. Huu utakuwa mkutano wa kwanza kati ya  Trump na Netanyahu  tangu kuanza kwa vita vya Iran, mada ambayo itagubika mazungumzo yao. Itakumbukwa kuwa katika miezi ya karibuni, Trump na Netanyahu walitofautiana kuhusu namna ya kuumaliza mzozo huo.

Hata hivyo Trump na Zelensky wamekutana mara kadhaa lakini rais huyo wa Ukraine amekuwa na wasiwasi kutokana na White House kuonekana kuitupilia Kyiv na kuelekeza nguvu zote katika mzozo wa Mashariki ya Kati.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW