SiasaIsrael
Netanyahu: Uhusiano wetu na Marekani ni madhubuti
29 Machi 2023Matangazo
Akizungumza kwa njia ya video katika mkutano wa kilele wa demokrasia ulioandaliwa na rais wa Marekani Joe Biden, waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema hana shaka na uthabiti wa demokrasia ya Israel, pamoja na urafiki usiotetereka na Marekani. Awali, Biden alikuwa amesema Israel haiwezi kuendelea na njia inayoichukua kwa sasa.
Netanyahu amesema ingawa wakati mwingine Israel na Marekani hutofautiana juu ya masuala kadhaa lakini uhusiano baina ya nchi hizo unaendelea kuwa imara. Jumatatu wiki hii Netanyahu alilazimika kuahirisha mpango huo wa mageuzi, baada ya maandamano makubwa na kuibuka kwa tofauti za wazi kati yake na maafisa wa ngazi za juu serikali akiwamo waziri wa ulinzi.