1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Netanyahu: Vita vya Gaza vina gharama kubwa kwa Israel

Hawa Bihoga
24 Desemba 2023

Waziri Mkuu wa Israel amesema leo kwamba vita katika Ukanda wa Gaza vimesababisha kile alichokiita "gharama kubwa" kwa jeshi la Israel huku idadi ya askari wa nchi hiyo waliouwawa katika mapigano na Hamas ikiongezeka.

Jeneza la sajenti Lavi Ghasi
Jeshi la Israel likibeba jeneza la sajenti Lavi Ghasi mjini ModiinPicha: Ariel Schalit/AP Photo/picture alliance

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameyasema hayo baada ya jeshi la Israel IDF kutangaza kwamba wanajeshi 14 wameuwawa katika ardhi ya Palestina kuanzia siku ya Ijumaa.

Katika taarifa yake, Waziri Mkuu huyo ameapa kuendelea na mapambano kwa nguvu hadi watakapofikia malengo yao ikiwemo kulitokomeza kundi la Hamas, kuwarejesha mateka na kuhakikisha Gaza si tishio tena kwa taifa la Israel.

Aidha ameweka wazi kwamba vita katika Ukanda wa Gaza itakuwa ya muda mrefu, hadi pale hali ya usalama itakaporejea katika maeneo ya Kaskazini na Kusini.

Tangu kuanza kwa mapigano hayo, jeshi la Israel limepoteza askari 153 huku pia likikabiliwa na mashambulizi mengine kutoka wanamgambo wa Hezbollah katika mpaka wake wa kaskazini na Lebanon.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW