1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Netanyahu yuko Washington kukutana na viongozi wa Marekani

24 Julai 2024

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu yuko mjini Washington DC ambako anatarajiwa kushiriki mikutano na viongozi wa Marekani na kuyahutubia mabaraza yote mawili ya Bunge la Congress.

Netanyahu na mkewe Sarah wakiwa njiani kwenda Marekani
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu yuko Washington DC ambako atakutana na viongozi wa MarekaniPicha: Amos Ben Gershom/Israel Gpo via ZUMA Press Wire/picture alliance

Netanyahu alitarajiwa kukutana na Rais Joe Biden Jumanne. Hata hivyo, mkutano huo uliahirishwa hadi Alhamisikwa sababu rais anaendelea kupata nafuu baada ya kuambukizwa UVIKO-19. Ikulu ya White House imesema Makamu wa Rais Kamala Harris -- anayeongoza katika mbio za kupata uteuzi wa chama cha Democratic kwa uchaguzi wa rais Novemba mwaka huu - atakuwa na mkutano tofauti na kiongozi huyo wa Israel. Aidha anatarajiwa kukutana na mgombea wa urais Mrepublican Donald Trump Ijumaa.

Netanyahu pia atayahutubia mabaraza yote mawili ya Bunge la Congress leo Jumatano, kufuatia mwaliko kutoka kwa viongozi wa mabaraza hayo. Spika wa Baraza la Wawakilishi Mrepublican Mike Johnson angependa sana kuonesha uungaji mkono wake kwa Israel.
Soma pia: Vikosi vya Israel vyaendelea kuushambulia Ukanda wa Gaza

Licha ya uungaji mkono unaoendelea kuoneshwa na Marekani kwa operesheni za Israel huko Gaza, mahusuano kati ya Netanyahu na Biden yameharibika. Idadi ya vifo huko Gaza inaendelea kupanda, na kufikia zaidi ya watu 39,000, wengi wao raia, kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Gaza inayoendeshwa na Hamas.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW