1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Neuer asema Bayern "wataiumiza" PSG

4 Novemba 2025

Mlinda lango mkongwe wa Bayern Munich, Manuel Neuer, amesema timu yake inafahamu pale pa kuiumiza Paris Saint Germain kuelekea mechi ya Ligi ya Vilabu Bingwa kati ya miamba hao wawili itakayochezwa leo.

Manuel Neuer | VfB Stuttgart vs FC Bayern Muenchen FCB
Picha: Weber/Eibner-Pressefoto/picture alliance

Neuer mwenye umri wa miaka 39 amesema hawaiogopi PSG na kwamba wanaelekea katika mechi hiyo kusaka ushindi.

Mlinda lango huyo ambaye ameshinda ligi hiyo mara mbili na Bayern anasema wana mpango maalum wa kuishinda PSG.

Mabingwa hao wa Ufaransa waliishinda ligi ya mabingwa msimu uliopita katika uwanja wa bayern, Allianz Arena walipoifedhehesha Intermilan 5-0, ila Bayern wanasafiri kuelekea nyumbani kwa PSG Parc des Princes wakiwa katika kiwango kizuri cha mchezo.

Bayern hawajapoteza mechi yoyote msimu huu wakiwa wameshinda mechi zote 15 walizocheza katika mashindano yote na wameweka rekodi ya mwanzo bora zaidi wa msimu katika ligi zote tano maarufu barani Ulaya.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW