1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Neuer asema hana haraka kuamua kuhusu mkataba wake na Bayern

4 Novemba 2025

Mlinda mlango wa Bayern Munich Manuel Neuer amesema hajaamuwa kama anataka kurefusha mkataba wake kwa mwaka mmoja mwingine katika klabu hiyo.

Manuel Neuer, mlinda mlango wa Bayern Munich na timu ya taifa ya Ujerumani
Manuel Neuer amekuwa katika klabu ya Bayern tangu mwaka wa 2011 na ameshinda mataji mengiPicha: Kai Pfaffenbach/REUTERS

Aidha, Neuer amesema hana haraka ya kufanya uamuzi wa kama anataka kuendelea kucheza kandanda akifika umri wa miaka 41. Akizungumza kabla ya mechi ya Jumanne usiku ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Paris Saint-Germain, Mjerumani huyo amesema kwa sasa ameelekeza fikra zake kwa kile kinachofanywa na timu yake.

Kwa sasa amesema ni mapema mno kwa sababu kuna mambo mengi yanayoweza kufanyika ikiwemo afya yake, na pia katika klabu ya Bayern kwa msimu ujao. Neuer atafikisha umri wa miaka 40 mwezi ujao wa Machi.

Amekuwa katika klabu ya Bayern tangu mwaka wa 2011 na ameshinda mataji mengi. Pia alishinda Kombe la Dunia la FIFA na timu ya taifa ya Ujerumani mwaka wa 2014 na kisha akastaafu mwaka jana. Kocha wake Vincent Kompany amesema Neuer hana haja ya kuwa na shinikizo lolote. Cha muhimu ni kwamba aendelee kucheza kandanda na kisha wakati ukifika atafanya uamuzi sahihi.