NEW DELHI: ajali ya treni yaua watu kadhaa India
29 Oktoba 2005Matangazo
Watu wasiopingua 35 wamekufa katika ajali ya treni iliyotokea kusini mwa India. Watu wengine 35 wamejeruhiwa .Ajali hiyo ilitokea baada ya treni hiyo ya abiria kuacha reli. Baadhi ya mabehewa yaliangukia katika sehemu zilizofurika.
Inasemekana watu kadhaa wamenaswa ndani ya mabehewa hayo yaliyomo ndani ya maji .Kila behewa lilikuwa na abiria kati ya 50 na sitini.Ajali hiyo ilitokea mapema leo asubuhi katika jimbo la Andhra Pradesh kusini mwa India.
.