NEW DELHI: India imefanya jeribio la kombora jipya
9 Julai 2006Matangazo
India imejaribu kombora jipya lenye masafa ya wastani na linaloweza kupachikwa kichwa cha kinuklia.Kombora hilo chapa ya Agni III lina uwezo wa kwenda umbali wa kama kilomita 3,000.Makombora ya aina hiyo yana uwezo wa kutoka India na kufika hadi Beijing na Shanghai nchini China.Mnamo mwezi wa Mei,waziri wa ulinzi wa India Pranab Mukherjee,aliarifu kuwa India ipo tayari kujaribu kombora hilo.Jeribio hilo limefanywa siku tano baada ya Korea ya Kaskazini kukosolewa vikali na jumuiya ya kimataifa kwa sababu ya kufanya majeribio ya makombora 7 katika Bahari ya Japan.