NEW DELHI: Rais wa kike wa kwanza nchini India
21 Julai 2007Matangazo
Rais mpya wa India ni Bibi Pratiba Patil wa chama tawala cha Congress.Patil ni mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo,baada ya kumshinda mpinzani wake,Bhairon Singh wa chama cha kizalendo cha Kihindu-BJP.Kura zilizosombwa na Bibi Pratiba Patil,ni maradufu ya zile alizopata mhasimu wake Bhairon Singh.