1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW DELHI: Rice ameianza ziara yake ya Asia

16 Machi 2005

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani.Bibi Condoleezza Rice amewasili mji mkuu wa India,New Delhi akiwa mwanzoni mwa ziara yake ya nchi sita za Asia.Leo atakutana na waziri mkuu wa India Manmohan Singh na waziri wa mambo ya kigeni Natwar Singh kabla ya kuelekea Pakistan jioni hii.Uhusiano wa kiuchumi na usalama,hali ya mambo nchini Nepal na utaratibu wa amani kati ya India na Pakistan ni baadhi ya masuala yanayotazamiwa kujadiliwa.Rice amepanga kuzizuru Afghanistan, Ujapani,Uchina na Korea ya Kusini vile vile.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW