NEW DELHI: Waasi wavamia vikosi vya usalama nchini India
24 Februari 2007Matangazo
Si chini ya wanajeshi 15 wameuawa baada ya kuvamiwa katika jimbo la Manipur,kaskazini-mashariki mwa India.Maafisa wanawashuku waasi wanaogombea kujitenga katika eneo hilo.Wamesema, kikosi maalum kinachopambana na uasi na kilichokuwa kikipiga doria,kilifyatuliwa risasi na wanamgambo katika wilaya ya Bishenpur inayopakana na Burma.Ripoti zinasema,zaidi ya watu 10,000 wameuawa katika uasi wa eneo hilo katika kipindi cha miongo miwili iliyopita.