NEW DELHI:Gambari asema atiwa moyo na India kuhusu suala la Myanmar
23 Oktoba 2007Matangazo
Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu suala la Myanmar Ibrahim Gambari amesema ametiwa moyo na ahadi zilizotolewa na India katika juhudi za kuunga mkono suluhu ya mzozo nchini Myanmar.
Matamshi hayo ya Gambari yametolewa baada ya mjumbe huyo kukutana na viongozi wa India ambao walikosolewa kutokana na kukaa kimya juu ya ghasia zilizofanywa na utawala wa kijeshi dhidi ya waandamanaji wa kutetea demokrasia wakiongozwa na watawa wakibudha huko Myanmar.
Gamabari yuko katika ziara ya mataifa ya Asia kujaribu kutafuta uungwaji mkono wa juhudi za Umoja wa mataifa katika kutia msukumo suala la mageuzi ya demokrasia nchini Myanamr.
Gambari baadae anaelekea China kwa lengo hilo la kuishawishi nchi hiyo kuukemea utawala wa kijeshi wa Myanamar.