NEW DELHI:Vifo vyaongezeka kwenye mafuriko Asia Kusini
3 Agosti 2007Matangazo
Idadi ya watu waliofariki inaongezeka kwenye eneo la Kusini mwa Asia kufuatia mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa za masika. Yapata watu milioni 20 wameachwa bila makao katika mataifa ya India,Bangladesh na Nepal.
Wahudumu wa misaada wanajitahidi kusambaza maji safi ya kunywa,chakula na dawa kwa wahanga wa mafuriko.Zaidi ya watu alfu 1 wamepoteza maisha yao katika eneo hilo tangu mwanzoni mwa msimu wa masika unaoanza katikati ya mwezi wa Juni kila mwaka na kusababisha mito kufurika.
Hii inasababishwa na kiwango kikubwa cha maji ya mvua na theluji inayoyeyuka kwenye milima ya Himalaya.