NEW YORK: Annan akutana na Pronk
27 Oktoba 2006Matangazo
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi amekutana na mjumbe wa umoja huo aliyefukuzwa kutoka Sudan, Jan Pronk. Pronk alifukuzwa na serikali ya Khatorum kwa kulikosoa jeshi la Sudan katika utendaji wake kwenye jimbo linalokabiliwa na vita la Darfur.
Jan Pronk aliamuriwa aondoke Sudan mwishoni mwa juma lililopita baada ya kuripoti katika tovuti yake binafsi kwamba jeshi la Sudan limepata hasara kubwa katika mapigano yake na waasi wa Darfur.
Serikali ya Khartoum ilihoji kwamba Pronk alijaribu kuongeza shinikizo kwa serikali ikubali majeshi ya Umoja wa Mataifa ya kulinda amani yapelekwe Darfur, ambako majeshi ya Umoja wa Afrika yameshindwa kukomesha umwagikaji wa damu.