1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK : Annan amependekeza mageuzi Umoja wa Mataifa

22 Machi 2005

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan amependekeza mageuzi mbali mbali katika chombo hicho cha dunia.

Akiuhutubia Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa mataifa mjini New York Annan amependekeza kutanuliwa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.Mageuzi hayo ni pamoja na kuanzisha kanuni za kutumia nguvu za kijeshi na kuongeza misaada kwa nchi zinazoendelea.Katibu Mkuu huyo amezitaka serikali kukubali mapendekezo yake hayo wakati watakapokutana katika mkutano wa viongozi wa dunia hapo mwezi wa Septemba.

Wakati Uingereza imesema inaunga mkono sana juhudi za Annan za kupunguza umaskini duniani Marekani imeelezea wasi wasi wake juu ya pendekezo la Annan la kuweka miongozo kwa ajili ya matumizi ya nguvu za kijeshi na nchi wanachama wa umoja huo kwa kusema kwamba ina mashaka na ufanisi wa hatua hizo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW