1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Annan atoa mwito kusitisha mapigano

21 Julai 2006

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Kofi Annan ametoa mwito wa kusitishwa moja kwa moja,mapambano yanayozidi kushika kasi,kati ya Israel na wanamgambo wa Hezbollah nchini Lebanon.Annan alitamka hayo katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa,alipokuwa akitoa ripoti ya tume ya Umoja wa Mataifa,iliyorejea New York kutoka Mashariki ya Kati.Annan amelaani mashambulio ya makombora yaliyofanywa na Hezbollah nchini Israel na kuwateka nyara wanajeshi wawili wa Kiisraeli.Vile vile amelaani kile alichokiita utumiaji wa nguvu wa Israel uliyopindukia kiasi.Marekani ambayo haijaonyesha ishara za kuishinikiza Israel,imesema waziri wake wa kigeni,Condoleezza Rice huenda akalizuru eneo la Mashariki ya Kati wiki ijayo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW