1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Annan kupongeza India na Pakistan

6 Januari 2004
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Kofi ANNAN amewasifu Rais Pervez MUSHARRAF wa Pakistan na Waziri Mkuu wa India Atal Bihar VAJPAYEE kufuatia mkutano wao wa jumatatu mjini Islamabad. Kikao hicho ambacho ni cha kwanza kati ya viongozi hao 2 kwa muda wa kiasi ya miaka 2 ulifanyika wakati Bwana VAJPAYEE akihudhuria mkutano wa viongozi wa nchi za kusini mwa Asia unaofanyika Pakistan. Nchi hizo 2 kubwa za Bara Hindi zenye nguvu za nuklia zimekuwa katika mvutano wa zaidi ya nusu karne kuhusu ugomvi wa jimbo la mpakani la Kashmir, na ambao umezusha vita mara 3 kati yao. Msemaji wa Bwana ANNAN amesema kuwa mkutano huo ni hatua muhimu yenye kusaidia kuimarisha uhusiano huo wa uhasama kati ya India na Pakistan.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW