1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK : Azimio kukomesha mapigano Lebanon laidhinishwa

12 Agosti 2006

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeidhinisha azimio lenye kutaka kukomeshwa kwa mapigano nchini Lebanon kati ya Israel na Hezbollah.

Azimio hilo linataka kukomeshwa kwa aina zote za uhasimu na kuruhusu uwekaji wa wanajeshi 15,000 wa Umoja wa Mataifa watakaosaidiwa na wanajeshi wa Lebanon wa idadi kama hiyo kudhibiti eneo la kusini mwa Lebanon wakati vikosi vya Israel vilivyolikalia kwa mabavu eneo hilo vitakapoondoka.

Akilihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hapo mwanzoni mwa mkutano wake hapo jana Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan ameshutumu kushindwa kwa baraza hilo kuchukuwa hatua na mapema ya kukomesha mapigano hayo na kusema kwamba jambo hilo limetingisha sana imani ya dunia kwa Umoja wa Mataifa.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condoleeza Rice ameahidi kulisaidia jeshi hilo la Umoja wa Mataifa.Baraza la mawaziri la Lebanon linatazamiwa kulizingatia azimio hilo leo hii lakini Rice amesema serikali ya Lebanon imemuhakikishia kwamba inaunga mkono maudhui ya azimio hilo.

Waziri Mkuu wa Israel Ehud Olmert pia amelikaribisha azimo hilo licha ya upinzani kutoka serikali yake.

New Zealand imesema iko tayari kutuma vikosi vyake vyake vya kulinda amani kusaidia Lebanon kulidhibiti tena eneo lake la kusini.

China,Japani na Australia pia zimeliunga mkono azio hilo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW