1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York. Balozi wa Iraq katika umoja wa mataifa alalamikia kuuwawa kwa binamu yake na majeshi ya Marekani.

2 Julai 2005

Balozi wa Iraq katika umoja wa mataifa ameyashutumu majeshi ya Marekani kwa kumuua mmoja kati ya binamu zake. Balozi Samir Sumaidaie amesema katika taarifa kuwa wanajeshi wa Marekani wamemuua binamu yake Mohammed Sumaidaie mwenye umri wa miaka 21 wakati wa msako katika nyumba yake hapo Juni 25 magharibi ya Iraq.

Balozi huyo ametaka kufanyike uchunguzi kuhusu mauaji hayo, akisema kuwa hasira juu ya mauaji hayo zinaweza kuathiri uungaji mkono wa raia kwa Marekani nchini Iraq.

Jeshi la Marekani limetoa taarifa yake, likisema kuwa madai ya balozi huyo yanafanana na tukio lililohusisha majeshi hayo katika siku hiyo na katika eneo hilo. Limesema uchunguzi utafanyika.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW