New York. Baraza haki za binadamu kutuma ujumbe Darfur.
14 Desemba 2006Matangazo
Baraza la haki za binadamu la umoja wa mataifa limekubali kutuma ujumbe katika jimbo lililokumbwa na mapigano la Darfur nchini Sudan.
Baraza hilo limesema kuwa ujumbe huo utajaribu kuchunguza madai ya kuporomoka zaidi kwa hali dhidi ya raia. Akizungumza siku ya Jumanne, katibu mkuu wa umoja wa mataifa Kofi Annan amesema kuwa ni muhimu kwa baraza hilo kujiingiza zaidi katika suala hilo la kusaidia kumaliza kile alichosema kuwa ni jinamizi la ghasia katika jimbo hilo.
Kiasi cha watu 200,000 wameuwawa na karibu watu wengine milioni mbili wamelazimika kuhama makaazi yao katika miaka mitatu ya mapigano kati ya majeshi ya serikali na waasi.