1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York. Baraza kuu la umoja wa mataifa laanza kikao cha 62.

19 Septemba 2007

Baraza kuu la umoja wa mataifa limeanza kikao chake cha 62 kwa wito uliotolewa na rais wake mpya wa kuimarisha uwezo wa taasisi hiyo ili kuweza kupambana na masuala mbali mbali ya kilimwengu.

Rais Srgjan Kerim kutoka Macedonia , ametoa wito wa kuimarishwa na kufanywa ya kisasa taasisi hiyo ya kimataifa ili kuweza kupambana na changamoto za karne ya 21.

Katibu mkuu wa umoja huo Ban Ki-moon amesema katika mkutano na waandishi wa habari kuwa Kerim ameamua suala la kupambana na mazingira kuwa mada kuu ya kikao hicho cha baraza kuu la umoja wa mataifa kwa mwaka mzima.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW