NEW YORK. Baraza la usalama kuzungumzia juu ya mswaada wa azimio la kusimamisha vita vya Lebanon
7 Agosti 2006Ndege za kivita za Israel zimefanya mashambulio katika viunga vya mji wa Beirut nchini Lebanon na kuwauwa watu 13 mapema leo katika sehemu zinazo aminika kuwa ziko chini ya udhibiti wa wapiganaji wa Hizbollah.
Majeshi ya Israel pia yalifanya mashambulio zaidi katika bonde la Bekaa karibu na mpaka wa Syria.
Wakati huo huo baraza la usalama la umoja wa mataifa leo hii litaanza tena mazungumzo juu ya mswaada wa azimio kuhusu kusimamisha mapigano baina ya Israel na wapiganaji wa Hizbollah nchini Lebanon.
Mswaada huo umewasilihswa na Marekani na Ufaransa.
Naibu waziri mkuu wa Israel Shimon Peres amesema.
O ton ….Huu ni mswaada wa azimio tu sisi tunasubiri litakapo pitishwa azimio ndio tutoe maoni yetu lakini ningetaka kukumbusha kuwa Israel imetimiza maazimio yote ya baraza la usalama la umoja wa mataifa juu ya Lebanon.
Lebanon imependekeza mabadiliko kadhaa katika mswaada huo uliopendekezwa na Marekani na Ufaransa.
Lebanon pia inasisitiza juu ya kuondoka kwa majeshi ya Israel kutoka nchini humo kama dai lake la kwanza.
Serikali ya Ujerumani imunga mkono mswaada huo ambao inasema ni hatua ya kwanza katika kumaliza mzozo wa Israel na Lebanon.