1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa larefusha mda wa jeshi la muungano nchini Irak

1 Juni 2005

Baraza la usalama la umoja wa mataifa limekubali kurefusha mamlaka ya jeshi la muungano nchini Irak. Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari baraza hilo limesema wanajeshi hao watabakia nchini humo hadi juhudi za kisiasa zikamilike. Serikali ya Irak yenyewe ndiyo iliyoliomba baraza hilo kurefusha muda wa kuwepo kwa jeshi hilo la muungano nchini humo.

Wakati huo huo, waziri wa mambo ya kigeni wan Iraq, Hoshyar Zebari ameitaka Marekani na mataifa mengine kuongeza misaada yao kwa Irak ili kupunguza kipindi cha kuendelea kuwepo kwa jeshi hilo la muungano. Zebari amepangiwa kukutana na waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice mjini Washington hii leo kujadili kuhusu kuongezwa kwa misaada.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW