1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK Baraza la usalama la umoja wa mataifa lashindwa kukubaliana kuhusu wahalifu wa kivita huko Darfur.

18 Februari 2005

Baraza la usalama la umoja wa mataifa limegawanyika kuhusu wapi kesi za uhalifu wa kivita uliofanywa katika eneo la Darfur nchini Sudan zinakotakiwa kuwasilishwa, huku Ulaya, China na Marekani zikitoa mapendekezo yao tofauti. Kwa mara ya kwanza wanachama 12 kati ya wanachama 15 wa baraza hilo, wanaunga mkono wahalifu wa kivita katika Darfur washtakiwe katika mahakama kuu ya kimataifa, The Hague, jambo linalopingwa na Marekani. China na Algeria zinataka serikali ya Sudan itumie mahakama zake na zinapinga kushtakiwa kwa wahalifu wa kivita katika mahakama hiyo ya kimataifa au katika mahakama maalumu itakayoundwa nchini Tanzania iliyopendekezwa na Marekani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW